Sunday, 27 July 2008

KIGOLI AINGIA MTINI

Kigoli cha jangwani kikimkimbia mnyama mkali

Klabu ya yanga leo iliingia mtini katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kombe la CECAFA kagame cup hivyo mahasimu wao Simba hivyo basi simba walijinyakulia nafasi hiyo ya tatu kwa bao 3 na pointi 3, lakini bado ni aibu hamna mcheza kwao hata mmoja fainali.

Saturday, 26 July 2008

WAKANADA HOI KWA USA

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya marekani wakishangilia ushindi dhidi ya Kanada mwenye nyeusi ni mzee mzima Lebron james ambaye ni majeruhi hivyo pengo lake anaziba Dwayne Wade


Katika game hiyo Dwyane Wade, Carmelo Anthony na Michael Redd swalichoma vikapu 20 kila mmoja wao kuwaadhibu Wakanada hapo Las Vegas. mpaka mapumziko walikuwa wakiongoza kwa 61-38 Kobe Bryant aliongeza pointi 15 , Deron Williams 14 na Chris Paul alichoma 11 na assist 8 , wakati wakanad a aliyejitahidi kidoga alikuwa Jermaine Anderson aliyeambulia pointi 18 pointshivyo hadi mwisho wa mchezo usa walishinda 120 - 65 .


Hii ilikuwa ni moja kati ya mechi zao za matayarisho kwa ajili ya olimpiki naona mwaka huu wana kikosi cha ukweli .

MARA NYINGINE TENA

Lewis Hamilton akishangilia ushindi

Lewis Hamilton aliwanyuka Heikki Kovalainen, Felipe Massa na Nelson Piquet katika dakika za mwisho na kufanikiwa kujisindia German Grand Prix huko Hockenheim Ujermani 21.07. Huu ni ushindi wake wa pili mfululizo na sasa anaongoza kwa pointi nne mbele ya Massa . Piquet alimaliza akiwa wa pili hii ni podium yake ya kwanza , Massa akiwa wa tatu wakati Kimi Raikkonen alikuwa wa sita

JANGWANI SASAMBU


Kikosi cha vijana wa jangwani


Timu ya Yanga jana iliyojitosa katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Tusker ya Kenya iliyofanyika Uwanja Mpya, Dar es Salaam jana , ilipigwa kimoko tu bila majibu 1-0. Hivyo sasa Simba na Yanga watakutana katika mchezo mshindi wa tatu ambaye atajinyakulia zaidi ya Sh milioni 12 , katika mchezo huo ambao utakuwa wa utangulizi kabla ya fainali ambayo itaikutanisha URA ya Uganda na Tusker ya Kenya, mshindi wa pili atachukua Sh milioni 23 na ushee na bingwa ataondoka na Sh milioni 34 hivi. Ni aibu hamna timu ya wenyeji fainali nahii inaweza kuzidi kutushusha katika msimamo wa soka duniani. AIBU

MNYAMA ANG'OLEWA MENO

Kikosi cha wekundu wa msimbazi

Timu ya Simba alhamisi hii iliyaaga mashindano ya baada ya kuchapwa 1 - 0 , na URA ya Uganda kama haitoshi kuonyesha kuwa mnyama huyo amekuwa wa kibisa sasa wakampa apige penalti ambayo ingewawezesha kurudi katika gemu mchezaji aliyetua siku si nyingi kisa ni mnigeria Izechukwu Emeh naye akamwaga hivyo mnyama nje.





Wednesday, 9 July 2008

NADAL AMZIMA FEDERAL

Nadal akishangilia ushindi wake

Rafael Nadal 22 alimpiga bao Roger Federal kujishindia mashindano ya Wimbledon kwa seti 3 - 2 , 6-4 6-4 6-7 6-7 9-7 baada ya mpambano huo uliochukua masaa 4:48 , na kuwa mspanish wa kwanza kutwaa taji hilo tangu 1966 alipochukua Manolo Santana's.

HAMILTON KIDEDEA


Lewis Hamilton (MCLAREN) Jumapili hii alijishindia British Grand Prix katika uwanja wa nyumbani Silverstone pamoja na hali ya mvua iliyokuwa ikiendelea na hivyo kuwa juu katika msimamo huo wa formula one katika mashindano hayo alifuatiwa na Nick Heidfeld (BMW )na watatu ni Ruben Barrichello (HONDA) , kwa matokeo hayo anaongoza msimamo akiwa na pointi 48 sawa na
Felipe Massa (Ferrari), Kimi Räikkönen

VENUS AMTOA NISHAI MDOGO MTU


Venus Willium alijishindia taji lake la tano la wimbledon katika fainali aliyokutana na mdogo wake Venus William kwa kumshinda 7-5 6-4 .
Wakina dada wakiwa pamoja

Wednesday, 2 July 2008

TIMU BORA DUNIANI

Shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza timu bora duniani na katika msimamo huo hispania kwa mara ya kwanza wamesimama katika namba moja. kma msimamo unavyoonyesha hapo chini nafasi nzao na kwenye mabano ni nafasi walizokuwa awali:
1. (4) Hispania, 2. (3) Italia, 3. (5) ujerumani, 4. (2) Brazili, 5. (10) Netherlands, 6. (1) Agentina, 7. (15) Croatia' 8. (6) Ucheki, 9. (11) Ureno, 10. (7) Ufaransa, 11. (24) Urusi, 12. (12) Romania, 13. (13) Cameruni, 14. (20) Uturuki, 15. (9) Uingereza, 16. (17) Skotlandi, 17. (18) Bulgaria, 18. (8) Ugiriki, 19. (14) Mexiko, 20 (16) Ghana, timu iliyoingia katika 20 bora ni Urusi na timu iliyotoka ni Colombia, Africa ya mashariki ni Kenya 92 nafasi 23 juu, Uganda 97 nafasi 2 juu, Tanzania ni115 nafasi 14 chini.

Tuesday, 1 July 2008

KILA KITU SPAIN

Mchezaji bora wa mashindano Xavi Hernadez.
Baada ya Euro 2008 sasa euro 2012 ni Poland Ukraine. Spain ndio kama vile wametoa gundu mabingwa wao vilevile Mfungaji bora ni wao David Villa, Mchezaji bora a mashindano ni Xavi Hernandez, wana wachezaji 9 bora katika timu ya mashindano,
Golikipa: Gianluigi Buffon (Italia), Iker Casillas (Spain), Edwin van der Sar (Uholanzi)
Mabeki: Bosingwa (Ureno), Philipp Lahm (Ujerumani), Carlos Marchena (Spain), Pepe (Ureno), Carles Puyol (Spain), Yuri Zhirkov (Urusi).
Viungo: Hamit Altıntop (Uturuki), Luka Modrić (Croatia), Marcos Senna (Spain), Xavi Hernández (Spain), Konstantin Zyryanov (Urusi), Michael Ballack (Ujerumani), Cesc Fàbregas (Spain), Andrés Iniesta (Spain), Lukas Podolski (Ujerumani), Wesley Sneijder (Uholanzi).
Washambuliaji : Andrei Arshavin (Urusi), Roman Pavlyuchenko (Urusi), Fernando Torres (Spain), David Villa (Spain).

Mfungaji bora David Villa


Wafungaji bora ni
4 -David Villa,

3 - Hakan Yakin, Semih Şentürk, Roman Pavlyuchenko, Lukas Podolski.

2 - Daniel Güiza, Ivan Klasnić, Zlatan Ibrahimović, Robin van Persie, Ruud van Nistelrooy, Nihat Kahveci, Andrei Arshavin, Wesley Sneijder, Arda Turan, Bastian Schweinsteiger,Fernando Torres, Miroslav Klose, Michael Ballack,

1 -Václav Svěrkos, Ivica Vastic, Klaas Jan Huntelaar, Rubén de la Red, Hélder Postiga, Ricardo Quaresma, Arjen Robben, Uğur Boral, Ivica Olić, Raul Meireles, Jan Koller, Dmitri Torbinski.

Magoli ambayo kila timu imejifungia ni :
12-Spain, 10-Uholanzi, Ujerumani, 8 - Uturuki, 7 - Ureno, Urusi, 5 - Croatia, 4 - Ucheki
3 - Sweden,Uswisi na Italia, 1 - Austria, Ufaransa, Ugiriki, Poland na Romania

MBONGO BINGWA WA DUNIA


Hii ilikuwa Jumapili tarehe 29.06.08 ndani ya Diamond jubilee ambapo mbongo japhet Kaseba ailshinda pambano hilo na kutetea ubingwa wa Dunia wa mchezo wa Kick Boxer, picha chini akiwa na mkanda huo wa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Chama cha Kickboxing Ulimwenguni (WKL), mara baada ya kumdunda mpinzani wake, Ricky Agayas kutoka Ufilipino katika raundi ya pili, katika ukumbi wa Diamond, Jubilee, jijini Dar pamoja nae ni baba yake Kaseba Matete kulia pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro.
karibuni wote ndani ya blog hii kwa michezo mbalimbali toka kila kona ya dunia