Sunday, 29 June 2008

SPAIN BINGWA

Wachezaji wa Spain wakishangilia ubingwa wao baada ya miaka 44 bila ya kombe lolote, hii ni baada ya kushinda bao 1 - 0 dhidi ya ujerumani, goli hilo la pekee lilifungwa na Fernando Toress.


Mwali ameenda spain.

Thursday, 26 June 2008

FAB AWAPELEKA SPAIN FAINALI


Wachezaji wa hispaniawakiongozwa na fundi au mtaalam kutoka The Gunners Cesc Fabregas kifua wazi wakishangilia ushindi wao wa bao 3- 0 dhidi ya warusi katika mechi ya nusu fainali , hapa watu uhakika wa kuingia fainali yao ya kwanza baada ya miaka 24, toka pale 1984 walipotinga fainali na kupigwa na wenyeji wafaransa bao 2 - 0 wafungaji wakiwa Michael Platini ambaye sasa ni raisi wa UEFA na Bruno Bellone, ambapo pia Platini alikuwa ni mfungaji bora akijiondokea na magoli 9 ambayo ni recod mpaka leo haijavunjwa , kati ya hayo 9 alikuwa na hat - tricks mbili dhidi ya Yugoslavia na Ubelgiji katika game hizo mbili alifunga magoli kwa style kwani kila game alihakikisha ana goli moja la kichwa, guu shoto na guu la kulia mtoto mtoto huyu aikuwa mbaya . Basi vijana wa Spain ndio vile tena mpaka jumapili dhidi ya wajerumani, magoli yao yalifungwa na Xavi Hernandez,Daniel Guiza na David Silva fabregas akitengeneza mawili pamoja na kuwa alikuwa akicheza nje ya nafasi yake ya kiungo, maana aliingia kama striker kuziba pengo la David Villa anayeongoza kwa magoli.

Wednesday, 25 June 2008

ujerumani fainali

Philiph Lahm akishangilia goli alilofunga dk za majeruhi kujihakikishia wanatinga fainali kwa kuwapiga bao 3 -2 wazee wa dk za mwisho uturuki

Monday, 23 June 2008

WATU WAMEVUNJA MWIKO

Cesc Fabregas anajitayarisha kwa nusu fainali baada ya kuisaidia timu yake kuishinda italia kwa mara ya kwanza katika mashindano tangu 1920, alimalizia penati yake kiufundi kuipa timu yake ushindi wa magoli 4 – 2 kwa penati baada ya timu hizo kumaliza muda wa nyongeza bila kufungana magoli na wenigne waliofunga kwa upande waSpain ni David Villa, Cazorla, Senna. Italia ni Fabio Grosso na Camoranesi... waliokosa niDaniele De Rossi na Di Natale.kwa ushindi huu timu ya spain imeondoa mkosi wake wa kufungwa tarehe za 22 june maana likuwa kama desturi yao 22.june.86 kombe la dunia walifungwa kwa penalty 5 -4 baada ya sare ya 1-1 baada ya kutoka 1 -1 dhidi ya Belgium, bao la spain lilifungwa na Juan Antonio Señor na Jan Ceulemans aliwafungia Belgium,penalti za Belgium zilifungwa na NicoClaesen, EnzoScifo, HugoBroos, PatrickVervoort na Leo Van Der Elst waliofunga kwa Spain ni Juan AntonioSeñor , Chendo, EmilioButragueño , Víctor Munoz na Eloy ndiye aliyemwaga,a lfu tena ikaja 1996 kombe la ulaya wakapigwa na England kwa ndani ya Wembley kwa penati baada ya kutoka suluhu penalti za Uingereza zilifungwa na Mtaalam Allan Shearer, David Plat, Stuart Pearce Paul Gasgoine gaza Hispania walifungiwa na Guillermo Amor, Alberto Belsue wakati waliomwaga ni Fernando Hiero, Miguel Ángel Nadal kama kawa 2002 tena wakapigwa na Korea ya kusini kwa penati 5 - 3 baada ya kutokufungana penati za wakorea zilifungwa na Hwang, Park ,Seol, Ahn na Hong wakati aWaspain walifungiwa na Fernando Hierro, Reuben Baraja na Xavi wakati Joaquin alikosa, Sasa picha linaanza kati ya Spain na final aliyebaki ni Urusi na kocha wa Urusi Guus Hidink ndiye aliyekuwa kocha wa Korea Kusini ilipoikung’uta Spain kumbuka, maana juzi tu ametoka kuiadhibu timuyake ya zamani ambayo wengi tulikuwa tukiipa nafasi kubwa Holand, tutaonana nusu fainali.

Sunday, 22 June 2008

PAUL INCE


Paul Ince 40 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha wa Blackburn Rovers kumrithi Mark Hughes (wote hawa ni watoto wa Sir Alex Ferguson). Kijana huyo wa Ilford atakuwa ni kocha Muingereza mweusi wa kwanza ndani ya Premiership, pia aliwahi kuwa muingereza mweusi wa kwanza kukaptain Uingereza ameitosa timu ya MK Dons ambayo msimu uliopita aliisaidia kupanda daraja na pia kushinda Johnstone's Paint Trophy. Ince aliwahi kuzichezea timu maarufu kama Manchester United, Liverpool na Inter Milan kabla ajajimix Middlesbrough , Wolverhampton Wanderers ambayo ilifanikiwa kupanda premier league kwa mchango wake mkubwa, Swindon Town alikuwa kocha mchezaji alafu akaenda Macclesfield Town kama kocha mchezaji ambapo aliwasaidia kutokushuka daraja , kabla ya kuhamia Milton Keynes Dons ambapo aliisaidia timu hiyo kupanda Coca-Cola League 1 mwaka huu.

MOTO GP

Casey Stoner amejishindia British MotoGP hapo Donington Park akimtangulia Muitaliano Valentino Rossi (Yamaha Factory) ambaye bado anaongoza msimamo wa mashindano hayo, watatu akiwa Dani Pedrosa (Honda HRC) wa Hispania aliyeanza mashindano hayo akiwa wa tisa, Muaustralia huyo Casey Stoner anawakilisha timu ya Ducati Moto GP.


Wakati huohuo Mika Kallio nae alijihakikishia kuendelea kuongoza msimamo wa 250cc World Championship aliposhinda kwa mbinde British MotoGP 250cc, hapo hapo Donington Park, ushindi huo ulikuja bila kutegemewaa kwani alianza mashindano hayo akiwa wa 14 akajitahidi kuwapunguza mmoko mmoko hadi robo ya mwisho aliwabakiza 2 mbele yake Alvaro Bautista na Marco Simoncelli ila zikiwa zimesalia lap 2 kama zali jamaa walijaa mmoja kushoto mwingine kulia mtu mzima akajipenyeza kati kama zali ndio vile tena.

FORMULA ONE


Filipe Massa ameshinda French Grand Prix huko Magny-Cours akifuatiwa na Kimi Raikkonen kuhakikisha timu yao ya ferari inajishindia namba moja na mbili, ambapo Jarno Trulli wa Toyota alijishindia nafasi ya tatu podium ya kwanza kwake msimu huu na ya kwanza kwa toyota tangu 2005, wakati ambapo Lewis Hamilton aliyeanza mashindano hayo katika nafasi ya 10 kama penalti kwa kumgonga kimi kizembe katika Canada GP alimaliza akiwa wa wa 11.

Khan bado bingwa


Bingwa wa Commonwealth uzito mwepesi Amir Khan jana alipita tena katika mtihani mgumu baada ya kufanikiwa kumshinda Michael Gomez katika raundi ya 5 ya mchezo huo, pichani juu Amir khan akisherehekea ushindi wake.

MOTO GP 125cc


Mutoto wa kiingereza Scott Redding leo amekuwa muingereza wa kwanza tangu 1986 kushinda mashindano ya pikipiki yanayoitwa Moto Gp 125cc katika uwanja wake wa nyumbani, akiwa na nashine yake ya Honda 125cc, alishinda kwa sekunde 5.3 baada yakuwa wa pili kwa muda mrefu wa mashindano hayo. Kijana huyo pia ameweka record kuwa mshindi akiwa na umri mdogo wa miaka 15 na siku 170.

Saturday, 21 June 2008

URUSI YATINGA NUSU FAINALI


Timu ya taifa ya Urusi imekuwa ya tatu kuingia katika hatua ya nusu fainali ya kombe la ulaya baada ya kuifunga timu ya Uholanzi kwa magoli 3 - 1, baada ya Dmitri Torbinski na Andrei Arshavin kunyakua goli moja moja katika dakika 8 za mwisho baada ya matokeo kuwa 1 -1, katika dakika 90 za mwanzo kabla ya muda wa nyengeza.

ETOO AWA MWIBA KWA STAZ

**********TANZANIA**************



Timu ya Taifa ya Cameroon Leo ilifanikiwa kutufunga kwa mbinde 2 - 1 katika mchezo uliofanyika kwao, baada ya Mchezaji wa kutumainiwa Samwel Etoo kufunga mabao yote mawili ,wakati ambapo bao la kufutia machozi la staa lilifungwa na Dan Mrwanda bao lililokuwa ni la ufundi wa hali ya juu.

Friday, 20 June 2008

UTURUKI YASHINDA KWA PENALTI

Waturuki wakishangilia ushindi wao wa (3 -1) kwa njia ya penalti baada ya kumaliza muda wa nyongeza wakiwa sare kwa goli 1-1 dhidi ya Croatia timu ambayo ilikuwa ikitegemewa kufanya vizuri katika mashindano haya ila naona pengo la mchezaji wao wa kutegemewa Eduardo De Silva wa Arsenal lilikuwa ni kubwa sana , Sasa Uturuki itakutana na Ujerumani katika nusu fainali .

Ujerumani 3 - 2Ureno



Timu ya taifa ya Ujerumani ilikuwa ya kwanza kuuingia Robo fainali kwa kuifinga timu ngumu ya Ureno mabao 3 - 0. Picha ni Bastian Schweinsteiger na Lukas Podolski nwakishangilia ushindi

Thursday, 19 June 2008

EURO 2008










**********************************EURO2008 *************************************************

Euro 2008 imeingia robo fainali na timu zilizobaki ni Ujerumani, Ureno, Croatia, Uturuki, Uholanzi, Uturuki, Hispania naI talia na mpaka sasa wafungaji bora kabla ya robo fainali ni
4 - David Villa - Spain
3 -Hakan Yakin - Switzerland , Lukas Podolski - Germany
2 - Arda Turan - Turkey, Zlatan Ibrahimović - Sweden, Nihat Kahveci - Turkey, Roman Pavlyuchenko - Russia, Wesley Sneijder - Netherlands, Robin van Persie - Netherlands
1 - Andrei Arshavin - Russia Michael Ballack - Germany Angelos Charisteas - Greece Cristiano Ronaldo - Portugal Rubén de la Red - Spain Daniele De Rossi - Italy Deco - Portugal Cesc Fàbregas - Spain Roger Guerreiro - Poland Daniel Güiza - Spain Petter Hansson - Sweden Thierry Henry - France Klaas Jan Huntelaar - Netherlands Ivan Klasnić - Croatia Jan Koller - Czech Republic Dirk Kuyt - Netherlands Luka Modrić - Croatia Adrian Mutu - Romania Ivica Olić - Croatia Christian Panucci - Italy Pepe- Portugal

Na hii ndio idadi ya magoli yaliyofungwa na kila timu ni
Holand 9, Spain 8, Portugal 5, Turkey 5, Croatia 4, Czech Republic 4, Germany 4, Russia 4, Italy 3, Sweden 3, Switzerland 3, Austria 1, France 1, Greece 1,Poland 1,Romania 1.




Wednesday, 18 June 2008

BOSTON CELTIC YAWALIZA LA LAKERS 131-92



















Wachezaji wa Boston Celtic wakishangilia ushindi wao dhidi ya Los angels Lakers walipowala katika game 6 kwa 131-92 na kujinyakulia kombe hilo kwa mara ya 17 hii ni record baada ya kulisotea kwa miaka 22.Picha kulia akiwa na kombe ni Paul Pierce ambaya pia ni MVP wa NBA Finals.




Nyota ichomozayo mchango wa kijana huyu katika finals ulikuwa ni mkubwa sana kama takwimu zinavyoonyeshaRajon Rondo
Points Rebounds Assist
Kg 20.4 Kg 10.5 RR 6.6
PP 19.7 KP 6.1 PP 4.6
RA 15.6 PP 5.0 KG 3.3
RR 10.2 RR 4.1 RA 2.7
KP- Kendrick Perkins
PP-Paul Pierce
KG-Kevin Garnett
RR-Rajon Rondo
RA-Ray Allen






"THE BIG THREE

Ray Allen
Kevin Garnet
Paul Pierce










karibuni wote ndani ya blog hii kwa michezo mbalimbali toka kila kona ya dunia