Sunday, 22 June 2008

PAUL INCE


Paul Ince 40 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha wa Blackburn Rovers kumrithi Mark Hughes (wote hawa ni watoto wa Sir Alex Ferguson). Kijana huyo wa Ilford atakuwa ni kocha Muingereza mweusi wa kwanza ndani ya Premiership, pia aliwahi kuwa muingereza mweusi wa kwanza kukaptain Uingereza ameitosa timu ya MK Dons ambayo msimu uliopita aliisaidia kupanda daraja na pia kushinda Johnstone's Paint Trophy. Ince aliwahi kuzichezea timu maarufu kama Manchester United, Liverpool na Inter Milan kabla ajajimix Middlesbrough , Wolverhampton Wanderers ambayo ilifanikiwa kupanda premier league kwa mchango wake mkubwa, Swindon Town alikuwa kocha mchezaji alafu akaenda Macclesfield Town kama kocha mchezaji ambapo aliwasaidia kutokushuka daraja , kabla ya kuhamia Milton Keynes Dons ambapo aliisaidia timu hiyo kupanda Coca-Cola League 1 mwaka huu.

No comments:

karibuni wote ndani ya blog hii kwa michezo mbalimbali toka kila kona ya dunia