Sunday, 22 June 2008

MOTO GP

Casey Stoner amejishindia British MotoGP hapo Donington Park akimtangulia Muitaliano Valentino Rossi (Yamaha Factory) ambaye bado anaongoza msimamo wa mashindano hayo, watatu akiwa Dani Pedrosa (Honda HRC) wa Hispania aliyeanza mashindano hayo akiwa wa tisa, Muaustralia huyo Casey Stoner anawakilisha timu ya Ducati Moto GP.


Wakati huohuo Mika Kallio nae alijihakikishia kuendelea kuongoza msimamo wa 250cc World Championship aliposhinda kwa mbinde British MotoGP 250cc, hapo hapo Donington Park, ushindi huo ulikuja bila kutegemewaa kwani alianza mashindano hayo akiwa wa 14 akajitahidi kuwapunguza mmoko mmoko hadi robo ya mwisho aliwabakiza 2 mbele yake Alvaro Bautista na Marco Simoncelli ila zikiwa zimesalia lap 2 kama zali jamaa walijaa mmoja kushoto mwingine kulia mtu mzima akajipenyeza kati kama zali ndio vile tena.

No comments:

karibuni wote ndani ya blog hii kwa michezo mbalimbali toka kila kona ya dunia