
Wachezaji wa hispaniawakiongozwa na fundi au mtaalam kutoka The Gunners Cesc Fabregas kifua wazi wakishangilia ushindi wao wa bao 3- 0 dhidi ya warusi katika mechi ya nusu fainali , hapa watu uhakika wa kuingia fainali yao ya kwanza baada ya miaka 24, toka pale 1984 walipotinga fainali na kupigwa na wenyeji wafaransa bao 2 - 0 wafungaji wakiwa Michael Platini ambaye sasa ni raisi wa UEFA na Bruno Bellone, ambapo pia Platini alikuwa ni mfungaji bora akijiondokea na magoli 9 ambayo ni recod mpaka leo haijavunjwa , kati ya hayo 9 alikuwa na hat - tricks mbili dhidi ya Yugoslavia na Ubelgiji katika game hizo mbili alifunga magoli kwa style kwani kila game alihakikisha ana goli moja la kichwa, guu shoto na guu la kulia mtoto mtoto huyu aikuwa mbaya . Basi vijana wa Spain ndio vile tena mpaka jumapili dhidi ya wajerumani, magoli yao yalifungwa na Xavi Hernandez,Daniel Guiza na David Silva fabregas akitengeneza mawili pamoja na kuwa alikuwa akicheza nje ya nafasi yake ya kiungo, maana aliingia kama striker kuziba pengo la David Villa anayeongoza kwa magoli.
1 comment:
I agree with you about these. Well someday Ill create a blog to compete you! lolz.
Post a Comment